Kahama FM
Kahama FM
September 21, 2025, 2:03 pm

”Wananchi wanapaswa kuelimishwa juu ya umuhimu ya kuchangia huduma ya maji ili kuwa na miradi endelevu ya maji”
Na Sebastian Mnakaya
Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira vijijini (RUWASA) Taifa Mhandisi Ruth Koya amewataka wananchi kuendelea kuchangia huduma za maji ili miradi iwe endelevu na yenye tija kwa wananchi hao.
Mhandisi Ruth ameyasema hayo katika ziara yake na wajumbe wa bodi hiyo, kukagua mradi wa maji wa pamoja (JWPP) baina ya serikali na mgodi wa dhahabu wa bulyhanhulu unaotekelezwa katika mikoa ya Shinyanga na Geita, katika kijiji cha Ilogi kata ya Bugala wilayani Kahama mkoani shinyanga.
Aidha amesema kuwa wananchi wanapaswa kuwaelimisha juu ya umuhimu ya kuchangia huduma hiyo, huku serikali kiendelea kutekleza miradi mbalimbali ya maji kwa wananchi wake ili kupata huduma hiyo kwa uhakika.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Mhandisi Wolta Kirita amesema kuwa serikali kupitia wizara ya maji ina mpango kwa kufikisha huduma ya maji vijiji vyote ifikapo mwaka 2030.

Nae Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Julieth Payovela, amesema Mamlaka imeendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maji ili wananchi wafikiwe na huduma hiyo, huku kukiwa na mpango mkakati wa kuchimba visima 900 ili kila kijiji kiwe na huduma ya maji.
