Kahama FM

Wafuga nyuki Ushetu watakiwa kuwatumia wataalam

August 17, 2025, 4:32 pm

Mkuu wa wilaya ya Kahama Frank Nkinda (Picha na Sebastian Mnakaya)

Ujenzi wa kituo hicho umegharimu kiasi cha shiringi milioni 84.8

Na Sebastian Mnakaya

Wafugaji wa Nyuki katika Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama mkoani Shinyanga wametakiwa kuwatumia wataalamu mbambili wa ufugaji wa nyuki ili kupata asili yenye ubora na yenye kuongeza thamani katika soko.

Agizo hilo limetolewa leo na Mkuu wa wilaya ya Kahama Frank Nkinda katika hafla ya kukabidhi jengo la kituo cha kukusanya mazao ya nyuki ulowa, ambapo jengo hilo limekabidhiwa kwa Chama cha Ushirika Cha Wafugaji wa Nyuki Ulowa (Ulowa Beekeepen Cooperative Society).

Aidha Nkinda amewataka wanancha wa ushirika huo kutunza na kulinda kituo hicho, huku akisisitiza wananchi kufuga nyuki ili kuongeza vipata vyao kwa kuongezewa thamani kupitia kituo hicho.

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Kahama Frank Nkinda
Mkuu wa wilaya ya Kahama Frank Nkinda akizundua jengo hilo

Nae meneja mradi wa kituo hicho Steven Paul amesema ujenzi wa kituo hicho umegharimu kiasi cha shiringi milioni 84.8, ambapo kukamilika kwake itawasaidia wafugaji wa nyuki kuleta asili katika kituo hicho na soko la uhakika.

Sauti ya meneja mradi kituo cha kukusanya mazao ya nyuki ulowa Steven Paul

Kwa upande wake mwenyekiti wa Chama cha Ushirika Cha Wafugaji wa Nyuki Ulowa (Ulowa Beekeepen Cooperative Society) John mganga Geriman ameishukuru serikali kwa kushirikiana na wawekezaji kwa kutekeleza mradi huo ambao utawasaidia kuongeza thamani ya asili na kuongeza vipato vyao.

Sauti ya mwenyekiti wa Chama cha Ushirika Cha Wafugaji wa Nyuki Ulowa (Ulowa Beekeepen Cooperative Society) John mganga Geriman

Kituo hicho kimejengwa kupitia mradi wa kuboresha Mnyororo wa thamani wa ufugaji wa nyuki (BEVAC) uliyokuwa unatekelezwa na shirika la Enabel chini ya usimamizi wa wizara ya Maliasi na Utalii kwa ufadhili wa umoja wa ulaya.