Kahama FM
Kahama FM
August 6, 2025, 8:31 pm

Mwenge wa uhuru umekagua na kuweka jiwe la msingi katika miradi sita katika halmashauri ya Msalala yenye thamani ya Bilion moja na Milioni tisini na tatu
Na Senastian Mnakaya
Jumla ya miradi sita ya maendeleo yenye thamani ya shilingi Bilion moja na Milioni tisini na tatu imekaguliwa, na imewekwa jiwe la msingi na wakimbiza mwenge wa uhuru katika Halmashauri ya Wilaya ya Msalala Mkoani Shinyanga uliokimbizwa leo Agosti 05, 2025 kwa km 32 wilayani humo.
Akiupokea mwenge huo wa uhuru kutoka Halmashauri ya Ushetu Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga ulikagua miradi 7 shilingi bililion 3.3 kwa kilometa 80, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Msalala Rose Manumba amesema miradi yenye thamani ya bilioni moja na milioni tisini na tatu itafikiwa na mwenge huo wa uhuru.
Miradi iliyofikiwa na mwenge wa uhuru ni ufunguzi wa nyumba ya mtumishi katika zahanati ya ntobo, kuweka jiwe la msingi ujenzi wa mradi wa maji kata ya Ntobo unaotekelezwa na RUWASA, ugawaji wa pikipiki za magurudumu mawili katika halmashauri ya msalala, kukagua ujenzi wa soko katika kituo cha mabasi Segese, kufungua shule shikizi iliyopo Segese, Na kuweka jiwe la msingi mradi wa matumizi ya nishati safi katika shule ya sekondari mwalimu nyerere.
Akiwa katika mradi wa Maji kata ya Ntobo Kiongozi wa Mbio za mwenge kitaifa 2025 Ismail Ali Usi anakiri kuridhishwa na ujenzi wa mradi huo, huku akiwataka wananchi kushiriki uchaguzi mkuu unaotarajiwakufanyika oktobamwaka huu.

Baadhi ya wananchi Melina Mwashela na Juma Mashimba wamesema mradi huo umewaepusha na adha walizokumbana nazo awali ikiwemo migogoro ya kifamilia, huku kukamilika kwa miradi hiyo itawasaidia kupata maji safi na salama kwa wakati.
Awali akisoma taarifa ya ujenzi wa mradi huo Meneja wa RUWASA Wilaya ya Kahama Mhandisi Magili Maduhu amesema mradi huo unatoa huduma kwa wananchi 1612 na milioni 88.3.
