Kahama FM
Kahama FM
August 6, 2025, 8:11 pm

Fedha za uwajibikaji kwa jamii (CSR) imefanikisha ujenzi wa soko la kisasa
Na Sebastian Mnakaya
Kampuni ya Barrick inazidi kutekeleza dhamira ya kuboresha maisha ya wananchi wanaoishi maeneo yanayozunguka migodi yake ya Bulyanhulu kupitia fedha za uwajibikaji kwa jamii (CSR) imefanikisha ujenzi wa soko la kisasa pamoja na matundu ya vyoo katika kata ya Segese, Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga kwa gharama ya shilingi milioni 304.
Hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi iliyoambatana na kutembelewa na mwenge wa Uhuru imefanyika katika soko hilo na kuhudhuriwa na wananchi kutoka vitongoji mbalimbali viongozi wa Serikali katika msafara wa mwenge na wafanyakazi wa mgodi wa Barrick Bulyanhulu.

Kiongozi wa Kitaifa wa mbio za Mwenge, Ismail Ali Ussi amesema Serikali inaendelea kujenga mazingira mazuri ya kuwakwamua wananchi kiuchumi mojawapo ni kuwawezesha wafanyabiashara wadogowadogo na wa kati kufanya biashara zao katika mazingira rafiki kama ambavyo limejegwa soko hili la Segese.
Awali, akisoma taarifa ya ujenzi wa soko hilo Afisa Mtendaji wa Kata ya Segese, Evamary Elias amesema ujenzi wa mradi huo umetekelezwa na mkandarasi ayesimamiwa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa kushirikiana na Halmashauri ya Msalala.

Baadhi ya Wananchi waliohudhuria katika hafla hiyo akiwemo GRACE William na Marry Peter wamepongeza Serikali na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa kuendelea kutekeleza miradi ya maendeleo katika wilaya yao.
Akizungumza kwa niaba ya Mgodi wa Barrick Bulyanhulu Kaimu Meneja Kitengo cha Mazingira na Uhusiano wa Jamii Zuwena Senkondo amesema kuwa mgodi utaendelea kutekeleza sera, sheria na kanuni zinazoletwa na serikali kama vile maudhui ya ndani (Local Content) na Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) kwa vitendo .

Ameongeza pia pamoja na mambo mengine mradi huo wa soko utasaidia kuboresha Mazingira ya kufanya Biashara na kuongeza kipato kwa wajasiliamali na wafanyabiashara wadogo wanaojihusisha na biashara sokoni hapo.