Kahama FM

Kahama waaswa kushiriki uchaguzi mkuu 2025

July 25, 2025, 4:13 pm

Mwanasheria wa kujitegemea Aisha Kitia kutoka SimbaNgwilimi Associates and Advocates( Picha na John Juma)

”Wananchi kudumisha amani na utulivu kwa kuchagua viongozi wanaowataka kwa ajili ya kutatua changamoto zao pamoja na kuleta maendeleo’

Na John Juma

Ikiwa imesalia miezi miwili kuelekea uchaguzi mkuu wa mwezi oktoba mwaka huu 2025, wananchi wa wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga wameaswa kushiriki vyema katika zoezi hilo ifikapo oktoba mwaka huu.

Kauli hiyo imetolewa leo na mwanasheria wa kujitegemea Aisha Kitia kutoka SimbaNgwilimi Associates and Advocates iliyopo kahama wakati akizungumza Kahama Fm, ambapo amewataka wananchi wanaokidhi vigezo vya kushiriki na kutimiza haki hiyo ya msingi kikatiba ya kupiga kura.

Sauti ya mwanasheria wa kujitegemea Aisha Kitia

Sambamba na hilo Kitia amewataka wananchi kudumisha amani na utulivu kwa kuchagua viongozi wanaowataka kwa ajili ya kutatua changamoto zao pamoja na kuleta maendeleo.

Sauti ya Sauti ya mwanasheria wa kujitegemea Aisha Kitia

Nao baadhi ya wananchi katika Manispaa ya Kahama akiwemo Honolasco Mfwambo, Ana Ngongi na Frank Raphael wakizungumza kwa nyakati tofauti wamesema kuwa kila mwananchi anapaswa kupiga kura kwa wale waliojiandikisha katika daftari la kudumu la mpiga kura ifikapo oktoba mwaka huu.

Sauti za wananchi Honolasco Mfwambo, Ana Ngongi na Frank Raphael

Uchaguzi Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hufanyika kila baada ya miaka mitano, kwa kuchagua viongozi mbalimbali wakiwemo nafasi ya Udiwani, Ubunge na Urais kwa mujibu wa katiba ya Tanzania