Kahama FM
Kahama FM
July 10, 2025, 4:51 pm

”Jamii kuchukua jukumu la kuwalinda watoto dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya na athari za mitandao ya kijamii kwa kutoa elimu kwa watoto wao’‘
Na Sebastian Mnakaya
Baraza la wazee manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga limeiasa jamii kuchukua jukumu la kuwalinda watoto dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya na athari za mitandao ya kijamii kwa kutoa elimu kwa watoto wao ili kuzuia mmomonyoko wa maadili.
Hayo yamesema na Mwenyekiti wa baraza hilo Laurent Nkwabi wakati akizungumza na Kahama fm katika ofisi za baraza hilo, ambapo amesema kuwa wazazi wanawajibu kuwafatili vijana wao kwa umakini ili wajiingize katika madwa ya kulevya.
Nao Baadhi ya wananchi Katika Halmashauri ya Manispaa ya Kahama Janeth James na Mussa Raphaeli wamesema kuwa mmomonyoko wa maadili unatokana na kupuuza mila na desturi za kitanzania na kuendekeza mila za kigeni na kwamba kila mtu ana jukumu la kuwalinda watoto hasa watoto wa kike.
Kwa upande wao baadhi ya vijana wakizungumza kwa nyakati tofauti akiwemo Aisha Shabani na Clementi Nalindo wamesema kuwa lawama hizo wanawatupia Lawama wazazi la walezi kuwa ndiyo chanzo.