Kahama FM
Kahama FM
June 14, 2025, 10:52 am

Wakulima wa zao la Tumbaku wamekabidhiwa pikipiki baada ya kufanya vizuri katika uzalishaji wa zao la Tumbaku
Na Leocadia Andrew
Kampuni ya ununuzi wa tumbaku Tanzania ya Alliance One imetoa pikipiki kwa wakulima bora wa zao la Tumbaku kwa mkoa wa kitumbaku Kahama, Tabora na Kasulu.
Zoezi la kuwapata washindi hao limefanyika wilayani Kahama kwa kuchezesha droo iliyotoa washindi kumi na tano wa zao la tumbaku.
Akizungumza mara baada ya kuwapata washindi hao afisa mahusiano wa kampuni ya Alliance One Paschal Songalimi amesema kuwa zawadi hizo walizotoa zimezingatia kiwango cha uzailishaji na kwamba lengo la kampuni yao inathamini mchango wa wakulima wa zao la tumbaku.

Akikabidhi zawadi hizo kwa niaba ya Mkurugenzi wa halmashauri ya ushetu Afisa kilimo wa halmashauri hiyo ambaye alikuwa mgeni rasmi katika Bahati nasibu hiyo Vaileth Rutakyamirwa ameipongeza kampuni ya Alliance One kwa kutoa hamasa hiyo kwa wakulima ambayo itawasaidia kuongeza juhudi katika kuendeleza kilimo cha tumbaku.
Naye mmoja wa washindi kutoka chama cha msingi Tulole Heneriko Mhoja amesema kuwa furaha yake ni kukubidhiwa pikipiki hiyo na ametoa shukrani kwa kampuni ya Alliance One kwa kuendelea kuwajali wakulima wake na kuwataka wakulima wengine kutokata tamaa na wazidi kuzalisha tumbaku kwa ubora.