Kahama FM
Kahama FM
May 8, 2025, 3:49 pm

”watumishi idara ya Mifugo na kilimo katika halmashauri ya Msalala wametakiwa kwenda kutekeleza utoaji wa chanjo hiyo kwa mifugo yote”
Na Sebastian Mnakaya
Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama mkoani Shinyanga imepokea zaidi ya dozi 82,000 ya chanjo ya Sokota kwa ajili ya mifugo ya Mbuzi na kondo.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa chanjo hizo mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Msalala Rose Manumba, amewataka watumishi idara ya Mifugo na kilimo tutekeleza utoaji wa chanjo hiyo kwa mifugo, huku mzalishaji wa chanjo hiyo Joseph Mapunda amesema watazambaza chanjo hiyo nchi nzima.

Mkuu wa idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi halmashauri ya Msalala Mfilinge Abdulikabili amesema kuwa wanachangamoto za ugonjwa Sokota hali inayosabashi kukosa soko ya nje kwa mifugo yao, pamoja na kuishukuru serikali kwa kutoa chanjo hiyo ili kuendana na kuapta soko la uhakika.
Kwa upande wake, Daktari wa mifugo kutoka halmashauri ya Msalala Ntano Kilagwile amesema kuwa ugonjwa huo unasababisha vifo vingi kwa mifugo na uzalishaji wake, huku serikali ikiwa na mkatati ya kupambana na magonjwa ya mifugo kwakuwa na kampeni ya mwaka mzima.

Serikali ya awamu ya sita inayoongzwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassani imeendelea kutoa chanjo mbalimbali nchini kwa ajili ya kupambana na magonjwa mbalimbali ya ya mifugo.