Kahama FM
Kahama FM
February 4, 2025, 5:08 pm

Na Marco Maduhu
Dawati la uchunguzi walipokea malalamiko 38,yaliyohusu rushwa ni 20 yasiyo husu rushwa ni 18, na kwamba uchunguzi wake unaendelea, huku akibainisha kuwa wamejipanga pia kuzuia vitendo vya rushwa kwenye uchaguzi mkuu ambao utafanyika mwaka huu 2025.
Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU)Mkoa wa Shinyanga,imeokoa kiasi cha fedha sh.milioni 137.8 za mauzo ya viwanja katika Manispaa ya Kahama,kutokana na baadhi ya watu waliomilikishwa viwanja hivyo kutolipa gharama halisi ya mauzo ya viwanja.
Hayo yamebainishwa leo na Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga Donasian Kessy wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari, kwa kipindi cha robo ya pili kuanzia Oktoba hadi Disemba 2024/2025
Amesema kwa kipindi hicho wamefanikiwa kuokoa sh.milioni 137.8 ikiwa ni sehemu ya fedha za mauzo vya viwanja 29 vilivyopimwa na Manispaa ya Kahama mwaka 2019, na kwamba katika viwanja hivyo ilitolewa gharama halisi ambayo wananchi wangepaswa kulipa, lakini viwanja vitatu (3) ndiyo vililipwa fedha halisi,huku 26 malipo yakiwa siyo sahihi.
Amesema baada ya kubaini hilo, waliweza kuwafikia wamiliki wa viwanja hivyo 26, na kuwataka walipe gharama halisi ya mauzo ya viwanja hivyo au vitangazwe upya
Ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Shinyanga, kwamba waendelee kutoa taarifa pale wanapoona viashiria vyovyote vya vitendo vya rushwa,ikiwa pamoja na miradi ya maendeleo ili hatua za haraka zichukuliwe.