Kahama FM
Kahama FM
February 3, 2025, 6:29 pm

Kilele cha Wiki ya Sheria ni kiashiria cha kuanza rasmi kwa shughuli za Mahakama ambapo kwa mwaka huu maadhimisho hayo yameongozwa na Kauli isemayo “Tanzania ya 2050, nafasi ya Taasisi zinazosimamia haki Madai katika kufikia malengo Makuu ya Dira ya Taifa ya Maendeleo”.
Na Sebastian Mnakaya
Watendaji katika taasisi mbalimbali za kimaamuzi wametakiwa kuzingatia weledi wakati wakitekeleza majukumu yao kulingana na mipaka na miongozo inavyowaelekeza.
Mkuu wa wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga Mboni Mhita Ametoa rai hiyo leo katika Kilele cha wiki ya sheria Wilaya ya Kahama ambapo amesema taasisi za kimaamuzi zikifanya kazi kwa kutozingatia mipaka inatengeneza migogoro ambayo haikubaliki.
Kwa upande wake Hakim Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Kahama Edmund Kente amesema kuwa moja ya Ufanisi katika Taasisi hiyo ni kuendesha Majukumu yake kwa Njia Mtandao ambao umesaidia kupunguza Mrundikano wa Mashauri ambayo hapo awali yalilazimu kutumia muda mrefu.
Wiki ya Sheria imehitimishwa leo ambapo kwa mwaka huu maadhimisho hayo yameongozwa na Kauli isemayo “Tanzania ya 2050, nafasi ya Taasisi zinazosimamia haki Madai katika kufikia malengo Makuu ya Dira ya Taifa ya Maendeleo”.