Kahama FM

“Wasio na NIDA kajiandikisheni mpate vitambulisho”

January 24, 2025, 10:44 am

baadhi ya vitambulisho vya taifa vinavyotolewa na mamlaka ya vitambulisho vya taifa NIDA

Kitambulisho cha Taifa ni nyaraka muhimu kwa mwananchi kutokana na kuonyesha utambulisho wa mwananchi.

Na Sebastian Mnakaya

Baadhi ya wananchi wa manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga wasiokuwa na vitambulisho vya Taifa wametakiwa kufika katika ofisi za NIDA kujiandikisha ili kupata vitambulisho hivyo.

Wito huo umetolewa leo na afisa uhamiaji wilayani Kahama Silieli Mchovu wakati akizungumza na Kahama FM , ambapo amesema vitambulisho hivyo ni muhimu ikiwemo pamoja na utambulisho wa muhusika.

Mchovu ameongeza kuwa vitambulisho hivyo ni muhimu katika shughuli mbalimbali za kila siku ambapo vinawasaidia kuaminika pamoja na kurahisisha katika kupata huduma mbalimbali katika taasisi za serikali.

Aidha Mchovu amesema kwa wale wenye vitambulisho vinavyohitaji marekebisho wanapaswa kufika katika ofisi za kata au za NIDA na marekebisho yatakapokamilika watajulisha kwa kutumia ujumbe .