Kahama FM

Mwili wa mwanamke wapatikana ukiwa umezikwa

January 18, 2025, 5:32 pm

Wananchi pamoja na jeshi la polisi Kahama wakishuhudia mwili wa mwanamke uliofukuliwa baada ya kuuawa na kuzikwa katika shimo

wachungaji wa ng’ombe walikuwa wanachunga katika maeneo hayo ndipo ng’ombe walikimbilia eneo hilo na kuanza kufukua, wachungaji waliwapiga ng’ombe ili watoke ndipo walipogundua kwamba kuna kitu kimefukiwa na kwenda kutoa taarifa

Na Sebastian Mnakaya

Mwili wa Mwanamke Asha Mayenga anayekadiriwa kuwa na miaka 62 alieuawa na kuzikwa Malindi Kata ya busoka Manispaa ya Kahama umefukuliwa na kutambuliwa na ndugu zake.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga, Janeth Magomi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akikiri kuwashikiliwa watuhumiwa watatu akiwemo mtoto wa marehemu

sauti ya kamanda Janeth Magomi

Aidha kamanda Magomi amebainisha chanzo cha mauaji hayo ni mgogoro wa ardhi baina ya marehemu na mtoto wake ambaye tayari anashikiliwa na jeshi la polisi,huku akitoa wito kwa wananchi kuacha kujishukulia sheria mikononi

sauti ya kamanda akielezea chanzo cha mauaji hayo

Kwa upande wake Mume wa marehemu Mashauri Mlekwa amesema alipewa taarifa za mke wake kupotea siku ya Jumatatu alipoenda shambani kulima na vijana wake.

sauti ya mume wa marehemu