Kahama FM

Dereva, utingo na abiria wafariki ajali ya malori kugongana uso kwa uso

August 15, 2024, 11:06 pm

Baadhi ya mabaki ya malori yaliyowaka moto picha na Sebastian Mnakaya

Watu watatu wamefariki dunia kwa kuteketea kwa Moto huku Wengine Watatu wakijeruhiwa katika ajali iliyohusisha Malori mawili kugongana uso kwa uso katika eneo la Manzese wilayani Kahama mkoani Shinyanga huku chanzo cha ajali hiyo kikitajwa kuwa Uzembe na Mwendokasi.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga SACP Janeth Magomi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambayo imehusisha Malori Mawili ya Mizingo Namba T 854 DBY lenye tela namba T 180 DVH likitokea Dar es salam kuelekea Lunzewe na Lori namba T 195 EEY Lenye tela namba T 811 DYU.

Sauti ya Janeth Magomi

Ajali hiyo imehusiha Malori Mawili ya Mizigo ambapo baada ya kugonga uso kwa uso yalianza kuwaka Moto na kusababisha vifo vya Dereva,Utingo na Mtu mwingine ambaye anaidawa kuwa ni abiria ambaye jina lake halifahamika mara mmoja.

Nao, baadhi ya mashuhuda wa ajili hiyo Denis Temba na Welnton Mngeja wakizungunza kwa nyakati tofauti wakiwa kwenye eneo la tukio maeleza namna ajali ilivyotokea kuwa zilikuwa kwenye mwendo kasi.

Sauti za mashuhuda

Kwa upande wake mkuu wa kituo cha Jeshi la Zima moto na uokoaji wilaya ya Kahama Hafidhi Omari ameelezea namna zoezi la uokoaji lilivyokuwa baada ya ajali hiyo.

Sauti ya kamanda wa jeshi la zimamoto