Kahama FM

Mtoto aliyepotea stendi ya mabasi Manzese Kahama apatikana

July 22, 2024, 6:14 pm

picha ya kamanda wa jeshi la polisi mkoani Shinyanga Janeth Magomi

Vitendo vya wizi wa watoto vinavyoendelea nchini kwa sasa, ni vema wazazi na walezi wawe waaangalizi wa karibu kwa watoto wao.

Na leokadia Andrew

Mtoto mwenye umri miezi 9 Meresiana Paschal,ambaye aliibwa katika Stendi ya Mabasi Manzese wilaya Kahama mkoani Shinyanga,amepatikana mkoani Geita akidaiwa kuwa na Binti Maduki Sabuni mwenye umri wa miaka (16).

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Janeth Magomi, amebainisha hayo leo wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari,ambapo amesema Julai 18 maeneo ya manzese wilayani Kahama,kulitokea tukio la mtoto wakati mama yake Magdalena Sulas (23) akiendelea na shughuli za utafutaji riziki katika stendi hiyo ya mabasi.

Amesema Jeshi la Polisi baada ya kupata taarifa za wizi wa mtoto huyo, lilianza kufanya upelelezi na kwamba Julai 21 mwaka huu, huko maeneo ya ushirombo wilayani Bukombe mkoani Geita, walifanikiwa kumkamata binti Maduki Sabuni (16) akiwa na mtoto huyo.

Aidha magomi ametoa wito kwa wazazi mkoani Shinyanga, kuwa wawe na uangalizi wa karibu kwa watoto wao.