Madiwani watakiwa kuhamasisha wananchi uboreshaji daftari la mpiga kura
July 4, 2024, 4:53 pm
vijana ambao tayari wamefikisha miaka 18 kujiandisha nao waweze kupata haki yao ya msingi ya kupiga kura
Na leokadia Andrew
Madiwani wa halmashauri tatu za wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga wametakiwa kuendelea kuwahamasisha wananchi kujiandikisha katika daftari la kudumi la wapiga kura katika kata zao katika kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mwezi oktoba mwaka huu.
Kauli hiyo imetolewa na kaimu mkuu wa mkoa wa shinyanga ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro wakati wa kikao cha baraza la madiwani katika kujadili hoja za mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG) wakati akimwalikisha mkuu wa mkoa wa shinyanga Anamringi Macha.
Aidha, Wakili Mtatiro wamewataka madiwani hao katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi wanapaswa ufanya mikutano ya mara kwa mara kwa wananchi, huku wakitakiwa kuendelea kuwaelimisha wananchi umuhimu wa kujiandikisha katika daftari la kudumu la mpiga kura ili waweze kushiriki kuwachagua viongozi wanaowataka.
Nae, diwani wa kata ya Nyahanga Pancreas Ikongoli, amesema mpaka sasa wanafanya mikutano kwenye kata zao kuwahamasha wananchi kujiandisha katika daftari hilo, huku wakiwataka vijana ambao tayari wamefikisha miaka 18 kujiandisha nao waweze kupata haki yao ya msingi ya kupiga kura.