Kahama FM

Wazazi, walezi simamieni maelekezo ya Mwenyezi Mungu katika familia

June 18, 2024, 4:31 pm

Shekhe mkuu wa wilaya ya Kahama Omary Damka

Wazazi wanapaswa kujitambua kwa kuwapelekea watoto wao katika shule zenye maadili pamoja na kuwasaidia jamii yenye uhitaji.

Na sebastian Mnakaya

Wazazi wilayani Kahama mkoani Shinyanga wametakiwa kusimamia na kuwalea vyema watoto wao katika maadili mema ya kumpendeza Mungu ili kuwa na familia bora pamoja na kuondokana na mmomonyoko wa maadili mema.

Agizo hilo limetolewa leo na shehe wa wilaya ya Kahama Omary Damka, wakati wa sala ya Eid Al Adha iliyosaliwa katika viwanja vya Taifa manispaa ya kahama, ambapo amewataka wazazi kuwalea vijana wao katika maadili mema kwa kuzingatia imani ya dini ya Kiisalamu.

sauti ya Shekhe mkuu wa wilaya ya Kahama Omary Damka

Kwa upande wao waaumini wa dini ya kiisilamu baada ya sala hiyo wamezungumza kwa nyakati tofautu, ambapo wamesema kuwa wazazi wanapaswa kujitambua kwa kuwapelekea watoto wao katika shule zenye maadili pamoja na kuisaidia jamii yenye uhitaji na kuwalinda watoto katika kipindi hihi cha sikukuu kutembea katika maeneo ambayo nafaa kwa watoto

sauti ya waumini wa dini ya kiisalmu