Kahama FM

Walimu shule za msingi na Sekondari jiandaeni kustaafu

June 12, 2024, 5:12 pm

katibu mwenezi wa chama cha mapinduzi wilayani Kahama Joachim Simbila {picha Sebastian Mnakaya }

Watumishi wengi wamesahau kujiajiri kipindi wapo kazini hali inayosababisha wakati wanastaafu kupata changamoto katika eneo la kipato

Na Sebastian Mnakaya

Walimu wa shule za msingi na Sekondari katika halmashauri ya Msalala wilayani Kahama mkoani Shinyanga wametakiwa kujiandaa kustaafu kwa kujishughulisha na ujasiliamali ili kupata kipato cha ziada baada ya ajira kufikia ukomo.

Kauli hiyo imetolewa leo na katibu mwenyezi wa chama cha mapinduzi (CCM) Joachim Simbila katika kikao kazi cha thamini ya elimu na wadau maendeleo kilichofanyika katika kata ya Segese kilichohudhuriwa na walimu wakuu wa shule za msingi na sekondari na maafisa elimu na viongozi mbalimbali wa serikali.

Sauti ya katibu Joachim Simbila

Naye, mthibiti mkuu wa ubora wa shule za halmashauri ya Msalala Raphael Ikombe amesema watumishi wengi wamesahau kujiajiri kipindi wapo kazini hali inayosababisha wakati wanastaafu kupata changamoto katika eneo la kipato, huku Mwalimu wa shule ya sekondari Ngaya Daniel Kabora ameeleza ambavyo walimu wanatakiwa kuwa na kipato cha ziada itakachowasaidia wakati utumishi wao ukifikia mwisho.

Sauti za walimu Msalala