Kahama FM

Wawili wachomwa moto kwa tuhuma za wizi Shinyanga

June 7, 2024, 9:11 am

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga Janeth Magomi

Vijana wawili waliofahamika kwa majina ya Bahati Dotto na Emma wakazi wa manispaa ya Shinyanga wamepigwa na wananchi wenye hasira kali na kisha kuchomwa moto hadi kupoteza maisha wakituhumiwa kujihusisha na matukio ya wizi.

Tukio hilo limeteokea jana mtaa wa Lwelyangula kata ya Kitangili ndani ya manispaa ya Shinyanga mkoani Shinyanga.

Akizungumza mwenyekiti wa mtaa wa Sanjo Musa Ramadhani amekiri kuwa mmoja kati ya vijana hao ni mkazi wa mtaa wake na amekuwa akijihusisha na shughuli mbalimbali ikiwemo ubebaji wa mizigo maeneo ya soko kuu mbali na tuhuma hizo huku majirani wa kijana huyo wakisimulia namna walivyokuwa wakiishi nae mtaani hapo.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga SACP Janeth Magomi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuahidi kuwasaka wale wote waliojihusisha na tukio hilo na kutoa rai kwa wananchi kutojichukulia sheria mkononi.