Emanuel Nyambi mwenyekiti mpya chama kikuu Cha ushirika Kahama (KACU)
June 2, 2024, 8:44 pm
wajumbe katika mkutano huo waliopiga kura jumla ni 282 kutoka vyama mbalimbali vya msingi kutoka katika halmashauri tatu za wilaya ya Kahama
Na Leokadia Andrew
Viongozi waliochaguliwa na wajumbe wa chama kikuu cha Ushirika (KACU) wilayani Kahama mkoani Shinyanga wametakiwa kufanya kazi kwa bidii na kuwa waadilifu pamoja na kuzingatia tararibu, kanuni na sheria za ushirika ili wakulima waweze kunufaika na ushirika huo.
Hayo yamesemwa na Mrajisi msaidizi mkoa wa Shinyanga HILDA BONIFACE, wakati wa uchaguzi wa wajumbe wa bodi na mwenyekiti wa chama hicho, ambapo amesema kuwa wanapaswa kuwatumikia vyema wakulima ikiwa pamoja na kulinda mslahi yao katika kipindi wawapo madarakani
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Kahama MBONI MHITA, amewataka viongozi hao waliochaguliwa kwa kipindi cha miaka mitatu kwa nafasi mbalimbali waende kusimamia kilimo cha pamba pamoja na kwenda na maono ya Rais SAMIA HASSANI katika suala la kilimo.
Nae, mwenyekiti mteule EMMANUEL NYAMBI amewashukuru wajumbe wa mkutano mkuu wa KACU kwa kumchagua kwa kura nyingi, nakuwahidi katika kipindi atakachokuwa madarakani atashugulikia changamoto za wakulima pamoja na kusimamia vyema chama hicho kwa manufaa ya wakulima
nafasi ya mwenyekiti ilikuwa na wagombea wawili TANO NSABI aliyepata kura 84 huku EMMANUEL NYAMBI akiwa mshindi kwa kupata kura 198.