Kahama FM

Magesa mbaroni kwa kumuua mtalaka wake

May 30, 2024, 10:36 am

Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Shinyanga Janeth Magomi
Mgogoro wa Talaka kati ya marehemu na aliyekuwa mumewe ambapo walikuwa na kesi Mahakamani juu ya Talaka ambayo ilikuwa itolewe hukumu yake May 28, 2024.


Na leokadia Andrew

Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga linamshirikia Jafari Magesa Miaka 31 Mkazi wa Milambo kwa tuhuma za kuunda njama za kumuua mtalaka wake na kitu chenye ncha kali aitwaye Gaudensia Shukuru miaka 25 Mkazi wa Malunga Manispaa ya Kahama.

Kamanda wa Polisi Mkoani Shinyanga Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi hilo Janeth Magomi amesema tukio hilo limetokea May 27 mwaka huu baada ya kupokea taarifa toka kwa Mwenyekiti wa kitongoji cha Wendele ya uwepo wa Mwili wa Mwanamke aliyeuwawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali

SACP Magomi amesema kuwa katika upelelezi wa awali wa chanzo cha tukio hilo ni Mgogoro wa Talaka kati ya marehemu na aliyekuwa mumewe ambapo walikuwa na kesi Mahakamani juu ya Talaka ambayo ilikuwa itolewe hukumu yake May 28, 2024.

Sauti ya kamanda Janeth Magomi