Kahama FM

Halmashauri ya Ushetu yapata hati safi

May 28, 2024, 5:28 pm

Mwenyekiti wa halmashauri ya Ushetu Gagi Lala akiwa katika baraza la madiwani (picha na Sebastian Mnakaya )

usimamizi wa ukusanyaji wa mapato umekwenda vizuri ukilinganishwa na mwaka wa fedha 2022/2023 ambao ukusanyaji ulikuwa mbovu mpaka kusababisha kupata hati chafu

na Sebastian Mnakaya

Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama mkoani Shinyanga imepata hati safi ambayo huku ukusanyaji wa mapato kwa vipindi vya robo ya pili na robo ya tatu vikiendele vizuri mpaka kufikia asilima 90%.

Baadhi ya madiwani wakizungumza katika kikao cha baraza la madiwani cha robo ya tatu ya mwaka, ambapo diwani wa kata Kinamapula SAMWEL ADRIAN amesema usimamizi wa ukusanyaji wa mapato umekwenda vizuri ukilinganishwa na mwaka wa fedha 2022/2023 ambao ukusanyaji ulikuwa mbovu mpaka kusababisha kupata hati chafu, huku diwani wa kata ya ukune PAUL MKOMBA akiomba ufafanuzi juu ya ongezeko la bajeti katika halmashauri hiyo.

Sauti za madiwani

Nae, mwenyekiti wa halmashauri ya Ushetu Gagi Lala, amesema baada ya halmashauri hiyo kukusanya mapato kwa asilimia 90% kwa robo ya pili hali iliyosababisha kuomba kuongeza bajeti ya shilingi bilioni 1.1 kwa ajili miradi ya maendeleo, huku akiwataka madiwani na matumishi kutimiza wajibu wao ili kuendelea kupata hati safi.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira Kulwa Shoto, akifafanua juu ya kuongezeko la bajeti hiyo kutokana na kupanda kwa kasi kwa ongezeko la mapato ya ndani kutoka asilima 44 hadi 104.

Hata hivyo, mwakilishi kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ibrahimu Makana amewapongeza madiwani na wataalum kwa ushirikiano ambao wanauonyesha nakufikia kupata hati safi na kujitahidi kufuta hoja inapoibuka.