Kahama FM

Wahudumu wa afya watakiwa kuwa na lugha nzuri

May 28, 2024, 12:56 pm

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Annamringi Macha amewataka watumishi wa idara ya Afya katika halmshauri ya msalala wilayani Kahama kuwa na lugha nzuri na zenye staha wakati wa kuwahudumia wananchi wanaofika katika vituo vyao kwa ajili ya matibabu.

Akizungumza na watumishi hao mara baada ya kukagua na kijionea huduma zinazotolewa katika hospitali hiyo, ambapo amesema wapo baadhi ya watumishi wasiofuata maadili na misingi ya kazi zao, hivyo ni vyema wachukuliwe ili wasichafue kazi nzuri inayofanywa na watumishi wengine waadilifu.

Aidha, ameutaka uongozi wa hospitali hiyo kuweka utaratibu maalum a kupokea maombi wa watu kupima afya zao (Medical checkup) ili kuwatengeneze wananchi desturi ya kujua afya zao bila kusubiria kuzidiwa.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha