Kahama FM

Wananchi Kijiji Cha Busangi kuanza kutumia maji ya Ziwa Victoria

May 1, 2024, 5:06 pm

Tanki la maji, miradi inayotekelezwa na RUWASA, (picha kutoka maktaba)

Mradi wa maji utakaowanufaisha Wananchi zaidi ya 10000 kata ya Busangi wenye thamani ya zaidi ya sh.bilioni 5

Na Sebastian Mnakaya

Zaidi ya wananchi 10,000 katika kata Busangi halmashauri ya Msalala wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga wamenufaika na mradi wa maji wa ziwa victoria wa Nduku Busangi wenye thamani wa shilingi bilioni 5.31 unaotekelezwa na wakala wa maji Safi na usafi wa mazingira vijijini RUWASA Kahama.

Wananchi wa kata hiyo wakizungumza mbele ya mkuu wa wilaya ya Kahama wakati wa akikagua mradi huo pamoja na kuuzindua wameishukuru serikali kwa kuwatatulia changamoto ya ukosefu wa maji, ambapo awali walikuwa wakitembea umbali mrefu

Sauti za Wananchi wa Busangi

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Kahama MBONI MHITA wakati akikagua mradi na kuuzindua amesema kuwa utakwenda kuwanufaisha takribani zaidi ya kata tano za halmashauri hiyo,huku akiwataka wananchi kutunza miundombinu ya maji na kutatua changamoto ya wananchi ya kutembea umbali mrefu kutafuta maji.

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Kahama Mboni Mhita

Kwa upande wake meneja wa wakala wa maji na usafi wa mazingira vijiji (RUWASA) wilaya ya Kahama Eng MADUHU MAGILI akitoa taarifa ya mradi huo, amesema usambaji wa mabomba ya chuma wenye urefu wa kilometa 18.92 umekamilika na maji yamefika katika kijiji cha Busangi na Nyamigege kwa gharama ya shilingi bilioni 2.98, na mradi umekamilika kwa asilimia 85% ambapo umetumia kiasi cha fedha shilingi bilioni 3.66.

Sauti ya meneja RUWASA Kahama