Kahama FM

Msalala yapokea shilingi mil 500 tozo, miamala ya simu

April 28, 2024, 5:58 pm

Picha ya mkuu wa wilaya ya Kahama mhe.Mboni Mhita

fedha zilizokuwa zinalalamikiwa na baadhi ya wananchi nchini za tozo na miamala leo zinatekeleza mradi miradi mbalimbali ya maendeleo

Na Sebastian Mnakaya

Serikali imeipatia halmashauri ya Msalala wilayani Kahama Mkoani Shinyanga kiasi cha shilingi milioni 500 kupita fedha za tozo na miamala ya simu kwa ajili ya utekelezaji mradi wa ujenzi wa kituo cha afya cha Mwalugulu ambacho kikikamilika kitaweza hudumia wananchi 23,631

Akisoma taarifa ya ujenzi wa kituo hicho mbele ya mkuu wa wilaya ya Kahama MBONI MHITA, kaimu mganga mfawidhi wa kituo hicho ESTER MWATWINA, amesema fedha zilizotolewa na serikali hazikutosha kukamilisha ujenzi huo, na hivyo halamshauri ya Msalala kupitia mapato ya ndani iliongeza kiasi cha shingili milioni 40 ili kukamilisha majengo hayo.

Sauti ya kaimu mkurugenzi Ester Mwatwina

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Kahama MBONI MHITA amesema kuwa fedha zilizokuwa zinalalamikiwa na baadhi ya wananchi nchini kuhusu tozo na miamala ya simu leo zinatekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo na mojawapo ikiwa ni kituo cha afya Mwalugulu.

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Kahama Mboni Mhita

Nae, mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya msalala HAMISI KATIMBA amesema kuwa wataendelea kutoa fedha za mapato ya ndani ili kuweza kukamilisha miradi mbalimbali, huku halmashauri hiyo ikiendelea kukusanya mapato kwa vyanzo mbalimbali kwa wingi.

sauti ya mkurugenzi mtendaji Hamis KATIMBA