KAHAMA:Jeshi la Polisi lawataka Wananchi kutoa taarifa za Uhalifu bila woga.
February 23, 2022, 1:01 pm
Jeshi la Polisi Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga limewatoa wasiwasi raia wema kuhusu utoaji wa taarifa za siri za waalifu katika maeneo yao kuwa wasiogope kama watajulikana pindi wanapotoa taarifa hizo.
Wito huo umetolewa leo na Mkaguzi msaidizi wa Polisi Joseph Kessy ambaye ni Msaidizi wa mkuu wa kituo cha Polisi Kahama wakati wa mahojiano maalumu na radio Kahama kuhusu hali ya uhalifu na waalifu manispaa ya Kahama.
Kessy amesema kuwa katika maeneo tunayoishi wapo wahalifu wengi ila jamii inasita kutoa taarifa kwa kuhofia kujulikana na kwamba jeshi la Polisi la Maboresho linatunza siri zote za taarifa za waharifu:
Sambamba na hayo Kessy amewataka wananchi kuelewa kuwa Utoaji wa dhamana kwa mhalifu ni haki yake ya msingi ila inategemea aina ya kosa na kwamba kuna kesi zingine haziruhusiwi kutoa dhamana.
Katika hatua nyingine amewataka wananchi waache uhalifu kwani biashara ya Uhalifu haiwezi kumfanya mtu afanikiwe kimaisha na badala yake utaishia kufungwa au kifo.
Nao baadhi ya wasikilizaji wa Kahama Fm wamelipongeza jeshi la Polisi kwa kazi nzuri wanayoifanya na wameomba kuwajua mapolisi kata wao na kupata mawasiliano yao.