Kahama:Viongozi na watendaji wa chama kikuu cha ushirika wilayani Kahama (KACU) wametakiwa kulinda heshima ya chama hicho.
January 22, 2022, 11:11 am
Viongozi na watendaji wa chama kikuu cha ushirika wilayani kahama (KACU) wametakiwa kuwa waaminifu wakati wakiwahudumia wakulima ili kulinda heshima na hadhi ya chama hicho.
Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya ya Kahama FESTO KISWAGA wakati akifungua kikao Cha mkutano mkuu wa 26 wa mwaka wa Chama hicho uliofanyika katika ukumbi wa KACU Mhongolo Manispaa ya Kahama.
KISWAGA amesema, lengo la kuanzishwa kwa ushirika lilikuwa ni kuwahudumia wakulima lakini baadhi ya viongozi wamekuwa wakitumia nafasi zao kujinufanisha, jambo ambalo hatavumilia kuona viongozi wa KACU wanadhulumu wakulima na kuhujumu ushirika.
Kwa upande wao Wajumbe wa mkutano huo wameiasa Bodi kuharakisha mchakato wa kupatikana fedha ili msimu ukianza Pamba inunuliwe kwa wakulima ili kuukabili ushindani wa wanunuzi wengine.
Hata hivyo,Chama hicho kimepitisha makisio ya ununuzi wa Pamba kwa msimu huu ambapo jumla ya kilo milioni 6, za Pamba zitanunuliwa kwa Shilingi bilioni 10 na milioni 800.