Benki ya CRDB yakanusha taarifa ya Kutoa zawadi Mitandaoni.
January 14, 2022, 7:32 am
Katika siku za hivi karibuni mitandao ya kijamii imetumika kama njia rahisi ya mawasiliano katika jamii.
Mitandao hii kuna wakati imekuwa ikitoa taarifa za kweli na kuna wakati imekuwa ikitoa taarifa za uongo zenye lengo la kuwaibia watu au kuzua taaruki.
Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na tangazo la Benki ya CRDB katika mitandao ya kijamii ikionyesha kuwa CRDB wanatoa zawadi kwa kujibu swali.
Taarifa hiyo ilikuwa na kichwa cha habari kisemacho CRDB Bank 25Th Annivesary.
Tazama linki hapa chini,
http://insidewhip.top/381aZ18BeV5jYVJUAUdSWVpzQl1YA2FZZ1tMJ2gBM18zLSIEcnQoISNUQDM?rfa1637299117928
Katika link hiyo ukifungua inaleta ujumbe huu
Congratulations!
CRDB Bank 25th Anniversary!
Through the questionnaire, you will have a chance to get 100000 Shilling .
Ikiwa na maana kwamba Hongera,Kwa kujibu dodoso utaweza fanikiwa kupata shilingi 100000.
UKWELI NI UPI?
Benki ya CRDB haijandaa utoaji wa zawadi kwa njia ya kujaza Maswali kama inavyoonekana hapo juu.
Kijukuu online Media imefanya mawasilinao na Meneja wa CRDB kanda ya Magharibi Jumanne Wagana na kuthibitisha kuwa Hiyo taarifa ni uzushi CRDB hawawahi kutoa Shindano hilo.
Pia Wagana amesema kuwa watanzania wanatakiwa kujifunza na kuzijua Links na Emails za Mashirikia na makampuni Mbali mbali ili watu wasiibiwe.
Wagana akaelezea kwa Undani kUhusu Email na Link kama inavyojieleza hapo chini.
*TUJIFUNZE KUHUSU HIZI LINKS NA EMAILS*
*Kwanza naomba nianze na maana ya hizi htpp:// na htpps://*
*htpp:// hii ambayo haina (s) mwishoni yaani http: hiyo hufahamika kama (hypertext tansfer protocol, hiyo kitaalamu Ni search engine inayotumika kutafuta au kukupeleka kwenye website fulani Sasa Ukiona umetumiwa link na imeanza na http: bila (s) mwishoni basi ujue hiyo sio salama*
*Hiyo (s) inakazi yake kubwa sana ambayo ni ulinzi wa taarifa kwa anaye bofya link*
*https: maana yake ni (hypertext transfer protocol secure)…..hapo utaona hiyo (s) kazi yake ni (secure) yaani ulinzi*
*Sasa links zote ambazo zina (http:) na siyo (https:) hizo zina viruses kwa lengo baya kwako*
*Hizi Links huwa zinatengenezwa kwa sababu mbalimbali na sababu kuu ikiwa ni kudukua (ku-hack) taarifa za watu*
*Na kwakuwa watu wanapenda vitu vya bure na rahisi basi huwa wanaandika utapewa zawadi pale utakapowatumia watu hiyo link*
*Sasa ukibonyeza hiyo link unaweza ukaambiwa weka namba zako za simu au email yako*
*Ukiweka hizo taarifa zako basi wao wanaweza kuchukua taarifa zako na kuweza kufuatilia mawasiliano yako au kukuibia pesa zako kwenye account zako zakifedha*
*Na Kama ulitumiwa link yenye (htpp:) kwenye Facebook au Instagram au mtandao mwingine wakijamii na ukabofya hiyo link maana yake HIYO ACCOUNT YAKO TAYARI WAMEISHIKILIA NA WAKATI WOWOTE WAKIAMUA WANAWEZA KUICHUKUA AU KUTUMA KITU CHOCHOTE KWENYE ACCOUNT YAKO*
*MUHIMU
*Email za kweli inapoandikwa, huwa likitoka jina la kampuni ndio linafuata neno kama vile (@gmail.co)*
Mfano Ukiona imeaandikwa (Coca-Cola@gmail.com) basi hiyo link ni ya Coca-Cola, lakini ukiona imeandikwa (Coca-Cola.money@gmail.com) hiyo email ni ya uongo, hivyo email ya kweli ni lazima ianze jina la kampuni au jina la mtu ndipo ifuate ile (@gmail.com) Ukiona umeandikiwa jina la kampuni halafu yakafuata maneno mengine, halafu ndio (@gmail.com), basi tambua huo ni wizi, mfano hata link ikiwa hivi (www.amazon.com), hiyo ni sahihi kwasababu Amazon ndio kampuni na ndio wamiliki wa link website hiyo hivyo kivyovyote vile taarifa zako ziko salama lakini ukiona (www.amazon.wd.com) hiyo sio yakweli maana tayari kuna vitu vimeongezewa hapo mbele
* Kampuni zote zinafahamu wateja wake zikitaka kutoa offer basi zitawafuata kupitia taratibu zao na sio kutuma links zenye viruses*
Mwisho:
Kwa ushahidi huo shindano la Benki ya CRDB halina ukweli wowote.