GEITA: LEAT yawapiga msasa madiwani 52 kuhusu sheria za madini na Utunzaji Mazingira.
November 22, 2021, 5:56 pm
GEITA
Madiwani wa halmshauri ya mji Geita Mkoani Geita wameiomba serikali na wadau wa maendeleo kuwapa elimu ya sheria ya ardhi na madini mara kwa mara ili kuwasaidia kuwa na uelewa kuhusu haki zao za msingi.
Madiwani wametoa Wito huo leo mkaoni Geita katika semina ya sheria ya uziduaji ya kuwajengea uwezo wa kuzitambua sheria za madini na ardhi katika maeneo yao wanayozunguka.
Nao baadhi ya madiwani wa viti Maalumu halmashauri ya mji wa Geita Winifrida Malunde na Evelina Mlyabuso wameiomba serikali kuwapa kipaumbele wanawake katika sekta ya uziduaji ikiwemo kuwapatia mikopo mikubwa ili iwasaidie katika uchimbaji wa madini.
Naye mwezeshaji wa semina hiyo kutoka timu ya wanasheria watetezi wa Mazingira (LEAT) wakili Baraka Thomas amesema kuwa semina hiyo imelenga kuwafundisha madiwani kuhusu utambuzi wa sheria za uziduaji na umiliki wa ardhi.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Busanda Tumaini Magesa amewashukuru Timu ya wanasheria watetezi wa Mazingira (LEAT) kwa kutoa semin hiyo kwani zitawafungua madiwani katika kujua sheria nyingi za ardhi na madini.
Semina hiyo ya mafunzo ya siku mbili iliyoanza Leo mkoani Geita imeandaliwa na timu ya wanasheria waetetezi wa Mazingira (LEAT) imejumuisha jumla ya madiwani 38 wa kata za halmashauri ya mji wa Geita na madiwani 13 waviti maalumu.