kahama
Kahama FM

KAHAMA:Watumishi wa serikali watakaokwamisha ujenzi wa Madarasa kusimamishwa kazi.

November 4, 2021, 1:49 pm

Walimu wa kuu shule za sekondari na watendaji wa serikali wilayani Kahama mkoani Shinyanga wametakiwa kusimamia vyema fedha za ujenzi wa madarasa zilizotolewa Rais SAMIA SULUHA HASSANI ili madarasa hayo yakamilike kwa wakati na watakaokwamisha watasimamishwa kazi.

Agizo hilo limetolewa na mkuu wa wilaya ya kahama FESTO KISWAGA katika ziara yake ya siku mbili katika Halmashauri ya ushetu,na kukagua shule za sekondari zilizopata fedha za Rais SAMIA HASSANI, ambapo amewata wakuu kukamilisha miradi ya ujenzi wa shule kwa wakati uliopangwa.

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Kaham Festo Kiswaga.

Kwa upande wake Afisa elimu sekondari Halmashauri ya Ushetu WENDELE WAKATALE, amesema kuwa kwa halmashauri hiyo imepokea takribani shilingi milioni 960 kwa ajili ya vyumba vya madarasa kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza watakaoanza mwaka 2022.

Sauti ya Afisa elimu sekondari Halmashauri ya Ushetu WENDELE WAKATALE

Nao, walimu wakuu wa shule za sekondari Halmashauri ya Ushetu wakizungumza na Kahama fm wameishukuru serikali kwa kutoa fedha hizo za ujenzi wa madarasa zitakazosaidia kuondoa msongamano kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza ifikapo January 2022.

Sauti za Walimu wakuu

Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania SAMIA SURUHU HASSAN ametoa fedha za ujenzi wa madarasa nchi zima ambapo Kwa wilaya ya kahama imepatiwa shilingi bilioni zaidi 6 ambazo zitajenga vyumba vya madarsa 267 kwa halmashauri tatu za ushetu, msalala na manispaa ya Kahama.