Kero ya barabara halmashauri ya Msalala yasababisha uwepo wa ajali nyingi.
August 30, 2021, 12:34 pm
Madiwani wa Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama mkoani Shinyanga wameiomba serikali kurekebisha miundombinu ya barabara ya Kahama hadi Kakola.
Madiwani hao wameleeza hayo katika kikao cha baraza la madiwani cha robo ya nne, wakati wa kipindi cha maswali ya papo kwa papo, ambapo wameeleza kuwa ubovu wa miundombinu katika barabara hiyo umepelekea uwepo wa ajali nyingi.
Kwa upande wake meneja wa wakala wa barabara za mijini na vijijini TARURA Halmashauri ya Msalala WILLFRED GUTTA amesema barabara hiyo ipo katika mkakati wa utekelezaji na suala hilo limefikishwa katika bodi ya barabara, ambapo maeneo ya miji midogo yatajengwa kwa kiwango cha lami.
Naye, Kamanda wa polisi halmashauri ya Msalala SSP KIONDO amewataka wananchi kufuata taratibu za barabara pamoja na kuacha matumizi mabaya ya barabara.