Watumiaji wa barabara watakiwa kuzingatia sheria na kanuni za barabarani Kahama.
June 8, 2021, 5:40 pm
Jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani Manispaa ya Kahama, mkoani Shinyanga limesema licha ya uchache walionao wanajitahidi kutoa elimu kwa watumiaji wa vyombo vya moto ili kuepusha ajali zinazotokea za mara kwa mara.
Akizungumza na KAHAMA FM mkuu wa kikosi cha usalama barabarani manispaa ya KAHAMA Inspekta WAMBURA amesema kuna maeneo mengi yenye changamoto ikiwemo eneo la LUMAMBO na MATAA kutokana na kutofuatwa kwa sheria za barabarani.
Amewataka watumiaji kuzingatia sheria za usalama barabarani na kwa yeyote atakayekamatwa atachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kutozwa faini na kufikishwa mahakamani.
Akizungumzia kuhusu kuharibika kwa taa za barabarani amesema waliohusika na uharibifu huo wamekamatwa na ukarabati umeanza katika maeneo ambayo taa zimeharibika.