Wazazi na waelezi katika Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga watakiwa kuwa wazalendo kwa kuwalea Watoto wao katika maadili.
June 8, 2021, 5:05 pm
Wazazi na waelezi katika manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga wametakiwa kuwa wazalendo kwa kuwalea Watoto wao katika maadili yaaliyo mema na kuwaonyesha njia sahihi ya kulitumikia taifa.
Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya ya Kahama ANAMRINGI MACHA wakati wa uzinduzi wa kituo cha maabara ya kisasa ya magonjwa ya binadamu cha MANJIS HEALTHCARE, ambapo amempongeza mkurugenzi wa maabara hiyo kwa uzalendo alionao kwa kufungua kituo hicho ambacho kitatoa huduma ya upimaji wa magonjwa mbalimbali kwa bei nafuu.
MACHA amesema kufunguliwa kwa maabara ya hiyo itarahisisha kwa mtu anayehitaji kupima magonjwa ambayo watu wengi imekuwa ikiwalazimu kwenda katika mikoa mingine kupata huduma ya upimaji na hata nje ya nchi.
Katika hatua nyingine mkurugenzi wa kituo hicho cha upimaji wa magonjwa ya binadamu MANJIS HEALTH CARE LIMITED Dkt.KUMAYL HUSSEIN PIRBHAI amewashukuru baadhi ya viongozi waliohudhuria katika hafla iyo fupi na kuwaahidi wananchi wa wilaya ya Kahama kutoa huduma bora.
Kituo cha maaabara ya kisasa ya magonjwa ya binadamu MANJIS HEALTH CARE LIMITED kimezinduliwa leo mjini Kahama ambacho kitatoa huduma zake za upimaji ikiwemo magonjwa ya moyo, saratani, figo,hormoni pamoja na ini .