MALENGO ENDELEVU
Kahama FM

UNA:Waandishi wa Habari zingatieni Malengo Ya Maendeleo Endelevu 2030 katika taarifa zenu.

May 11, 2021, 4:12 pm

DAR ES SALAAM

Waandishi wa Habari hususan wa redio za kijamii nchini wametakiwa kutumia malengo ya maendeleo endelevu 2030 katika kuibua changamoto mbalimbali zilizopo katika jamii zao kwa lengo la kuleta ufumbuzi na kuwakumbusha wasimamizi na watunga sera.

Semina Ikiendelea katika Ukumbi wa Seascape Hotel Jijini Dar es salaam.

Hayo yamesemwa leo na Afisa Programu wa shirika la (UNA) Goodluck William wakati akiongea na waandishi wa Habari wa redio za kijamii zinazoshiriki mradi wa uchechemuzi kwa njia ya  vipindi vya redio vinavyoangazia maswala ya maendeeo na jinsia vinavyodhaminiwa na shirika lisilo la kiserikali za Policy Forum.

William amesema kuwa ili kuboresha vipindi vya redio ni muhimu kutumia malengo ya maendeleo endelevu 2030 kwa jambo husika kwa kuwa ni malengo ambayo yanagusa jamii nzima kwa maslahi ya Taifa na watu wake.

Sauti ya Goodluck William akisisitiza waandishi wa habari Kutumia malengo ya maendeleo endelevu 2030 katika kuandaa vipindi.

Kwa upande wake Afisa Msimamizi wa masuala ya Jinsia kutoka Shirika Lisilo la kiserikali la Policy Forum Iman Hatibu ametoa wito kwa waandishi wa Habari kutumia kalamu zao kuandika Habari nyingi za maswala ya kijinsia kwani makundi mengi ya kijamii yamesaulika katika jamii.

Sauti ya Afisa Msimamizi wa masuala ya Jinsia kutoka Policy Forum Iman Hatibu.

Nao baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo Bashiru Mohamed  kutoka redio Safari Mtwara na Fatma Buriani kutoka Mashujaa Fm Wamelishukuru shirika la Policy Forum kwa kuwapa mafunzo hayo na kwamba swala la malengo ya maendeleo endelevu walikuwa hawalifahamu kwa undani licha ya kwamba wameshafanya vipindi vingi vya jami vyenye mlengo huo.

Suati ya baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo.

Shirika la Policy Forum limeandaa mpango mkakati wa miaka minne ambao umelenga kuleta usawa katika kugawa huduma za kijamii na utawala unaoshirikisha wananchi.