Kikosi cha 23 KJ Kimehitimisha mafunzo rasmi ya Sambalatisha Adui.
April 29, 2021, 10:08 am
Jeshi la wananchi wa Tanzania kikosi cha 23 KJ limehitimisha mafunzo rasmi ya sambalatisha adui yaliyolenga kujikumbusha mbinu mbalimbali za kivita ikiwa ni pamoja na kujiweka timamu kila wakati ili kuendelea kulinda mipaka ya nchi .
Mkuu wa shule ya ifantiria Brigedia Jenerali Selemani Gwaya ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mazoezi hayo ,amewataka askari walioshiriki mafunzo hayo kuendelea kufanya mazoezi zaidi kwa kuzidisha muda wa kuwepo kambini ili kujiweka timamu na kuhakikisha mipaka ya nchi inakuwa salama
Kwa upande wake kamanda wa vikosi vya magharibi Brigedia Jenerali Julius Gambusi amesema mafunzo hayo wamepata uzoefu ,katika maeneo ya mbinu za kivita ,uvumilivu ,utimamu wa mwili na usimamizi wa vikundi katika ngazi mbalimbali.
Nao baadhi ya askari walioshiriki mafunzo ya sambalatisha adui kwa mwaka 2021 Luteni Ussu Melania Rwekiiza ,Luteni ussu Happyness Paulo Luteni ussu Fatuma Othman wamesema wamefurahishwa na mazoezi hayo ambayo yamefanyika kwa vitendo huku wakiahidi kuendelea kujinoa zaidi