Serikali Wilayani Kahama Yaipongeza Benki ya TPB Kwa kutoa madawati 92 Ushetu.
April 15, 2021, 4:32 pm
SERIKALI Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga imeishukuru Benki ya Posta Tanzania (TPB) Kwa kujali na kutumia faida yake waliopata kuirudisha kwenye jamii kwa kutoa jumla ya madawati 92 katika Shule ya Sekondari Ubagwe Halmashauri ya ushetu.
Akizungumza mara baada ya kupokea madawati hayo,Mkuu wa Wilaya ya Kahama ANAMRINGI MACHA amesema benki hiyo imetoa sehemu ya faida yake katika ili kusaidia shule hiyo ambayo ilikuwa na mapungufu ya vyumba vya madarasa na madawati.
MACHA ametoa wito kwa wazazi na wananchi kuendelea kushirikiana na Serikali katika ujenzi wa maboma ya shule hiyo pasipo kusubiri kukumbushwa na Rais au waziri mkuu wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwa upande wake,Mkurugenzi wa Mikopo wa Benki TPB HENRY BWOGI amesema kuwa benki yao imekuwa ikishirikiana na serikali kutoa faida wanayopata kwa ajili ya kurudisha fadhila kwa jamii katika Nyanja ya Elimu na Afya.
Naye Mwalimu mkuu wa shule ya Sekondari Ubagwe MAGEMBE LUCAS ameishukuru benki ya TPB kwa msaada huo na kwamba Shule ya Ubagwe ina idadi kubwa ya wanafunzi na ilikuwa na upungufu wa madawati zaidi ya 60.
Benki ya Posta tawi la Kahama (TPB) imeanzishwa mwaka 2013 na imekuwa ikitoa misaada mbalimbali kwa jamii hususan katika Nyanja ya Afya na elimu.