Adhana FM

Waandishi wa habari Zanzibar wametakiwa kufanya uchechemuzi ili kuchochea kurekebishwa vifungu vya sheria kandamizi dhidi ya uhuru wa haabri.

10 February 2023, 4:31 am

Na Ali Khamis, Zanzibar

Waandishi wa habari Zanzibar wametakiwa kupaza sauti zao kwa mamlaka zinazohusika kuondoa  vifungu vya sheria kandamizi katika tasnia habari nchini ili kuimarisha uhuru wa kujieleza na ukuaji wa demokrasia kwa maendeleo nchini.

Wito huo umetolewa katika mafunzo ya siku mbili yaliyofanyika Zanzibar katika kuendeleza ya mradi wa boresha habari, yaliyondaliwa na Chama cha waandihi wa haabri wanawake TAMWA Zanzibar kwa kushirikiana na shirika la Internews na Ubalozi wa matekani yametolewa ili kuwajenga wandishi katika kutafuta mwafaka wa vifungu mbali mbali vya kisheria vinavyo minya ukuaji wa vuandishi wa habari nchini.

Mkufunzi wa shule ya uandishi wa haabri ya Chuo Kikuu Cha Taifa Cha Zanzibar SUZA Iman Duwe, amefafanua vifungu  vya sheria za habari vinavyokizana na uhuru wa vyombo vya habari na kujieleza ambapo amewataka waandishi kuvifayia kazi kwa kuieleza jamii kutokana na kueba maslahi mapana iwapo vifungu hivyo vitarekebishwa.

Alieleza  kuwa zipo sheria kuu mbili za habari ambazo ni sharia ya usajili wa wakala wa habari, magazeti na vitabu ya mwaka 1988 na sharia namba nane tume ya utangazaji ya mwaka 1997 ambazo bado kuna vifungu vinakwamisha uhuru wa habari hapa Zanzibar na iwapo waandishi hawatasimama  imara kwa kupaza sauti zao, kutakua na tatizo katika tasnia ya habari kwa baadhi ya vifungu hivyo vintoa mamlaka makubwa kwa waziri kufungia chombo cha habari au kuunda bodi ambazo zinaweza kuwa na wajumbe wasiofahamu vyema maslahi ya vyombo vya habari.

Mkufunzi kutoka shirika la magazeti Zanzibar Juma Khamis Juma alisema kuwa ili kuleta uchechemuzi ambao utachochea kasi ya mabadiliko katika jamii,   wanahari wanatakiwa kufafanua  kifungu kwa kifungu badala ya kuangalia mapungufu ya sheria kwa ujumla.

Alikitolea mfano kifungu cha 16 (1) sheria ya baraza la wawakilishi, kinga uwezo na fursa, sheria namba 6 ya 2022, kimempa spika uwezo wa kutoa hati ya kumlazimika shahidi kuhudhuria mbele ya baraza au kamati jambo ambalo ni vyema lingeachwa katika mamlaka ya mahakama ili baraza nalo lingechukua fursa ya kufungua mashtaka mahakamani ili kila muhimili wa nchi kufanyakazi zake.

Naye mkurugenzi wa TAMWA Zanzibar, Dkt Mzuri Issa alisema kuwa wandishi wa haabri waendelee kufanya ushawishi katika kuhimiza mabadiliko ya sheria zenye mapungufu ili ipatikane sheria itakayoweka mazingira bora kwa vyombo vya habari vya Zanzibar.