Adhana FM

Makamo wa Kwanza wa Rais: Walimu Shirikianeni na taasisi kupambana na unyanyasaji wa watoto

30 September 2021, 5:17 am

Makamu Wa Kwanza Wa Rais Wa Zanzibar Othman Masoud Othman, Amewataka Walimu Kushirikiana Na Taasisi Mbali Mbali Katika Kuandaa Mkakati Shirikishi Utakaongoza Na Kusimamia  Mapambano Dhidi Ya  Unyanyasaji Wa Watoto.

Akifungua Kongamano La Walimu Huko Katika Ukumbi Wa Sheikh Idrissa Abdul-Wakil Kikwajuni Mjini Zanzibar, Ikiwa Ni Matayarisho Ya Kuelekea Kilele Cha Siku Ya Waalimu Duniani, Itakayofanyika Tarehe 5 Oktoba Ameipongeza

Wizara Ya Elimu, Nakuahidi Kwamba Serekali Itashirikiana Na Chama Cha Walimu Zanzibar, Katika Kuzipatia Ufumbuzi Changamoto Zao.

Akimkaribisha Mgeni Rasmi Waziri Wa Elimu Na Mafunzo Ya Amali Zanzibar, Mhe. Simai Muhamed Said, Amewataka Walimu Waliokusanyika Katika Kongamano Hilo Kuaandaa Mbinu Mbadala Katika Kuwasaidia Wanafunzi Nakuwajengea Uwezo.

Akisoma Risala Ya Chama Hicho  Mwalimu Haji Juma Omar, Amemuomba Makamu Wa Kwanza Wa Rais Kuwasaidia Katika Kufanya Maboresho Ya Sheria Ya Elimu Zanzibar Ili Kuendana Mahitaji Ya Sasa.

Kongamano Hilo Lenye Kaulimbiu Ya Mwalimu Ongoza Mapambano Dhidi Ya Unyanyasaji Wa Watoto, Limehudhuriwa Na Wadau Mbali Mbali Wakiwemo Walimu Wastaafu.