Vwawa FM Radio
Vwawa FM Radio
January 9, 2026, 10:26 am

Kwa malengo ya kuongeza ubora wa taaluma
Na Devi Moses
SERIKALI imeahidi kuendelea kuboresha na kuendeleza Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam(DIT) Kampasi ya Songwe ili kuongeza ubora wa mafunzo ya ufundi nchini.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Daniel Mushi,amesema hayo Januari 8, 2026, wakati wa mahafali ya 19 ya duru ya tatu yaliyofanyika katika Kampasi ya Songwe.
Mushi ameipongeza DIT kwa juhudi zake za kuwatambua wabunifu na kuwaendeleza ili waweze kuchangia kikamilifu katika maendeleo ya taifa.
Awali, Mkurugenzi wa DIT Tanzania, Prof. Preksedisi Ndomba, amewataka wahitimu kwenda kuchapa kazi na kuuza ujuzi walioupata
Akitoa salamu kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mkuu wa Wilaya ya Momba, Mhe. Elias Mwandobo, amewahimiza wahitimu hao kuunda vikundi na kuanzisha kampuni.