Vwawa FM Radio

ADP Mbozi lawataka watoa huduma za afya wajifunze lugha ya alama

June 7, 2025, 7:47 am

Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya lugha ya alama wakimsikiliza mtoa mada. Picha na Stephano Simbeye

Ni kurahisisha mawasiliano na wasiosikia

Na Stephano Simbeye

Shirika lisilo la Kiserikali la ADP Mbozi mkoani Songwe limewasihi watoa huduma za afya nchini kuielewa lugha ya alama inayotumiwa na wenye changamoto za kusikia ili waweze kuwasiliana vuziri na watu wanaotumia lugha hiyo wanapohitaji huduma.

Ofisa Mradi wa ADP Mbozi, Maneno Uledi alisema hayo alipozungumza kwenye mafunzo maalum kuhusu lugha ya alama ambayo yalifanyika mjini Vwawa Juni 6.

Alisema lengo la mafunzo hayo ni kuwapa uelewa watoa huduma za afya Ili wafahamu namna ya kuwasiliana na watu wenye changamoto za kimawasiliano wanapofika kwenye vituo vya matibabu.

Sauti ya Maneno Uledi

Uledi alisema mradi huo umedhaminiwa na shirika la DSW na ni mwaka mmoja na nusu ambapo ADP Mbozi ni mtekelezaji wa mradi huo.

Alisema hadi sasa mradi umefikia asilimia 93 ya malengo yake kwa kuwafikia vijana 4,236 kati ya 4,560 waliokusudiwa.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo Ofisa vijana halmashauri ya Mbozi, Rolandi Mponzi aliwataka washiriki kuwa wasikivu ili kupata kilichoandaliwa kwa usahihi.

Sauti ya Rolandi Mponzi