Vwawa FM Radio
Vwawa FM Radio
May 7, 2025, 11:54 am

Ni kutaka kuwaridhisha wateja
Na Anyisile Freddy
Wauzaji wa gesi ya kupikia wametakiwa kuwa na mizani ya kupimia mitungi ya gesi ili kulinda uaminifu kwa wateja.
Mfanyabiashara wa kuuza mitungi ya gesi mjini Vwawa mkoani Songwe, Grace Sichone amesema hayo Mei 6, 2025 alipozungumza na Vwawa Fm.
Amesema kwa kawaida mtungi mdogo mtupu unazo kilo 8, na gesi inayojazwa ni ya kilo 6, hivyo mtungi wenye gesi unatakiwa kuwa na jumla ya kilo 14.
Naye mteja wa mitungi ya gesi Mariamu Malanga akizungumzia suala hilo ameunga mkono , akisema baadhi ya watumiaji hawatunzi vizuri mitungi yao hali inayosababisha kuchafuka haraka.