Uyui FM

DC Tabora azindua dawati la uwezeshaji biashara

27 September 2025, 7:31 pm

Na Wilson Makalla

Mkuu wa wilaya ya Tabora, Upendo Wella amezindua Dawati Maalum la Uwezeshaji Biashara kwa Wananchi mkoa wa Tabora siku ya Jumanne Septemba 23, 2025 katika Ofisi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA ) Mkoa wa Tabora na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali pamoja na Wafanyabiashara mkoani humo.

Akizungumza katika hafla hiyo, amewataka watendaji wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) watakaokabidhiwa ofisi hiyo kuhakikisha wanasikiliza wananchi na kutatua changamoto zao kwa weledi.

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Tabora, Upendo Wella.

Kwa upande wake Meneja wa TRA mkoa wa Tabora, Fredrick Kanyilili amesema ofisi za dawati hilo zitapatikana katika ofisi zote za TRA mkoani humo hivyo amewataka mameneja wa wilaya kuongeza ushirikiano na serikali za mitaa hasa maafisa biashara katika wilaya na watendaji wa kata ili waeze kuwatambua na kuwatambua wajasiriamali wadogo na kuwaelimisha ili watambue umuhimu wa kulipa kodi.

Sauti ya Meneja wa TRA mkoa wa Tabora, Fredrick Kanyilili

Akizungumza kwa niaba ya wajasiriamali na wafanyabiashara, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake Tabora, Ashura Mwazembe amesema wanashukuru kwa kuzinduliwa kwa dawati hilo na kuahidi kulitumia kikamilifu ili kupata ujuzi na fursa zilizopo katika kukuza biashara zao na kujikwamua kiuchumi.

Sauti ya Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake Tabora, Ashura Mwazembe

Uzinduzi wa Dawati hilo ni utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan la kuanzisha Dawati Maalumu la Uwezeshaji Biashara katika mikoa na wilaya zote nchini.