Uyui FM

TAKUKURU Tabora yatahadharisha vitendo vya rushwa kipindi cha kampeni

9 September 2025, 6:57 pm

Na Zabron G Balimponya

Wananchi mkoani Tabora wametakiwa kuacha tabia ya kupokea zawadi  au fedha kutoka kwa wagombea wa vyama vya siasa kwani ni kinyume cha sheria.

Mkuu wa kitengo cha uelimishaji umma Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rusha  (TAKUKURU)  mkoa wa Tabora Happiness Madege ,amesema hayo wakati akizungumza na UFR.

Mkuu wa kitengo cha uelimishaji umma Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rusha  (TAKUKURU)  mkoa wa Tabora Happiness Madege akizungumza katika studio za Uyui FM Radio

Sauti ya Mkuu wa kitengo cha uelimishaji umma Takukuru Tabora Happiness Madege

Wananchi Manispaa ya Tabora wameeleza uelewa wao juu ya utambuzi wa viashiria vya rushwa.

Maoni ya Wananchi Tabora kuhusu viashiria vya Rushwa

Vyama mbalimbali vya siasa vinaendelea kunadi sera zao kwa wananchi ili kuomba ridhaa ya kuchaguliwa ifikapo Oktoba 29 mwaka huu.