Wanafunzi wa Ruchugi watumia saa mbili kufika shule
12 January 2025, 4:38 pm
wameeleza athari wanazokutana nazo wakati wa kwenda shule na kurudi nyumbani kutokana na kutembea umbali.
Na Linda Dismas
Wanafunzi katika shule ya sekondari Ruchugi, wilayani uvinza mkoani kigoma, wameeleza jinsi ambavyo wanatembea umbali mrefu wa masaa mawili kufika shule kunavyowaathiri katika masomo yao.
Hayo yamesemwa na baadhi ya wanafunzi shuleni hapo wakati wakizungumza na uvinza fm, nakusema kuwa wanawaomba viongozi wa shuleni hapo kupunguza gharama za bweni ili kuwasaidia katika masomo yao na kuongeza ufaulu.
Nao baadhi ya wazazi kijijini humo wameeleza namna ambavyo watoto wao wamekuwa wakikabiliwa na changamoto barabarani zinazopelekea kushindwa kukamilisha masomo yao.
Sambamba na hayo, wameeleza jinsi ambavyo wamejipanga kukabiliana na tatizo hilo.
Aidha walimu shuleni hapo wameelema kuwa wanafunzi wamekuwa wakipata changamoto kitaaluma kutokana na umbali mrefu kati ya shule na nyumbani.
Pia wametoa wito kwa serikali na sekta binafsi na wadau wa elimu kuboresha Barbara na kungeza mabweni ili kuwaepusha wanafunzi na athari hizo na badala yake kuongeza ufaulu.