Wafanyabiashara waishukuru serikali kwa kuondoa vikwazo vya kufanya biashara
19 August 2021, 4:45 pm
Na,Glory Paschal
Wafanyabiashara katika halmashauri ya mji wa Kasulu mkoani Kigoma wameishukuru serikali kupitia mamlaka ya mapato Tanzania TRA kuondoa vikwazo vya kufanya biashara vilivyokuwa vinawakabili ikiwemo kubabikiziwa makadilio ya juu ya kodi na baadhi ya watumishi wasio waadilifu.
Wamesema tangu walipofanya mgomo kwa kufunga maduka wakiomba watumishi wa mamlaka ya TRA kubadilishwa ikitokana na kubambikiziwa makadilio ya juu ya kulipa kodi, kwa sasa mamlaka imewasikiliza na kutatua kero na sasa kwamba biashara zinafanyika kwa uhuru.
Kwa upande wake Meneja wa mamlaka ya mapato mkoa wa Kigoma Gabriel Mwangosi amewataka wafanyabiashara kuweka kumbukumbu sahihi za biashara ambazo zitaepusha wao kubugudhiwa na mamlaka hiyo na kulipa kodi kwa wakati.