Tumieni michezo kupinga vitendo vya udhalilishaji
13 July 2024, 7:48 am
Jamii inapaswa kuitumia michezo kama njia ya kupinga udhalilishaji.
Na Abdul Sakaza.
Wadau wa kupinga vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia Zanzibar wametakiwa kuitumia michezo mbalimbali katika kupinga vitendo hivyo ndani ya jamii zao.
Ameyasema hayo huko uwanja wa michezo Mau Zedong’s Stadium Mratibu Wa Mradi wa Michezo kwa Maendeleo kutoka Jumuia Ya Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA ) Bi Rufea Juma katika mafuzo yaliohusisha michezo kwa vitendo ambayo imewashirikisha wadau mbali mbali wa kupinga vitendo vya udhalilishaji hapa zanzibar.
Bi Rufea Amesema ikiwa wadau wa kupinga vitendo hivyo watatumia fursa za michezo kikamilifu katika kupinga na kutoa elimu kwa jamiii itasaidia kupunguza ukatili na unyanyasaji kwa wanawake na watoto kwani michezo inanafasi kubwa ya kupunguza kasi ya vitendo hivyyo katika jamii tunazoishi
Picha na Abdul Sakaza.
Picha ya mkufunzi wa masuala ya kimichezo Makame Amir Mgeni akiwa na wanamichezo mbali mbali.
Kuipa michezo kipao mbele hasa kwa vijana kunanafasi kubwa ya kuzuwia udhalilishaji.
Kwaupande wake Mwalimu wa Wichezo na Mtaalamu wa michezo kwa maendeleo hapa Zanzibar Ndugu Makame Amir Mgeni amesema michezo inanafasi kubwa ya kuviondoa kabisa vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia katika jamii kwani vinatoa fursa kujiamini,kujitambua na kuimairisha akili ya mtoto
Nao washiriki wa mafunzo hayo wamelishukuru Jumia Ya Wanasheria Wanawake Zanzibar kwa kuwapa mafuzo mzazuri huku wakiahidi kuitumia michezo katika kupinga vitendo hivyo ndani ya jamii zao