Tumbatu FM

Sakaza: Changamoto za wakulima lazima zitatuliwe

8 July 2024, 9:29 am

Mbunge wa jimbo la Chaani Ndugu Juma Usonge. Picha na Abdul Sakaza.

Iwapo serikali itatatua changamoto zinazowakumba wakulima kutawawezesha kuvuna mazao mengi zaidi.

Na Abdul Sakaza.

Mbunge Wa Jimbo La Chaani Mhe. Juma Usonge ameishauri Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Waskazini Unguja kutatua changamoto za wakulima wa bonde la Mpunga Kibokwa ili kufikia lengo la serikali kupitia sekta ya kilimo hapa nchini.

Ameyasema hayo hii leo katika kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja kilichofanyika Mahonda katika ofisi za chama hicho, kikao ambacho kilikuwa na lengo la kusikiliza utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM juu ya miradi mbali mbali ya maendeleo ambayo imefanya na serikali.

Aidha amewashauri viongozi wanaosimamia sekta ya kilimo kufanya utafiti wa mabonde ya kilimo ili kufahamu aina ya kilimo kinachotakiwa kulimwa katika maeneo hayo jambo ambalo litasadia kuleta mapinduzi ya kilimo kwa wakulima.