Tumbatu FM
Tumbatu FM
2 March 2026, 12:43 pm

Jeshi la polisi kupitia dawati la jinsia Mkoa wa Kaskazini Unguja limiepanga kupeleka walimu wa usalama wetu kwanza katika skuli za Tumbatu ili kutoa elimu kuhusu masuala ya udhalilishaji wa kijinsia.
Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa dawati hilo Sajent Salum Khamis Machano wakati wa kikao cha Pamoja kati ya walimu wa skuli ya sekondari Tumbatu Pamoja na kamati ya wazazi kuhusu changamoto ya ukatili wa kijinsia kisiwani humo.
Amesema wamepokea malalmiko kutoka kwa wasamaria wema kuhusu kuwepo kwa baadhi ya watu wa eneo hilo wanaofanya vitendo vya kuwadhalilisha watoto jambo ambalo limewafanya kuweka mikakati itakayopelekea kuliondosha tatizo hilo ikiwemo kuwapeleka polisi watakaosaidiana na walimu kutoa taaluma kwa wanafunzi.
Aidha amewataka wazazi kuwa na tabia ya kufuatilia mienendo ya watoto wao Pamoja na kutowapa uhuru wa kupiliza jambo ambalo hupelekea kuongezeka kwa matendo mabaya.
Kwa upande mwengine mwenyekeiti wa kamati ya wazazi skuli ya sekondari Tumbatu Mwalimu Ngwali Mkame Kire amaekiri kuwepo kwa vitendo vya udhalilishaji katika
jamii huku akisema changamoto kubwa ni kutoviripoti kwa mamlaka husika kutokana na ukaribu wa kifamilia.
Nao wajumbe wa kamati hiyo wameliomba jeshi la polisi kuharakisha upatikanaji wa walimu wa usalama wetu kwanza sambamba na kupelekea elimu kwa walimu wa madrasa.