Kahama FM

Wananchi watakiwa kuhifadhi chakula

May 27, 2024, 11:11 pm

Picha ya mazao aina ya mahindi, miongoni mwa mazao yanayolimwa na wananchi wa uUshetu(picha kutoka maktaba)

Wafanyabiashara wengi wamekuwa wakinunua mazao kwa bei ya chini hali inayosababisha wakulima kuuza chakula na kusahau kukihifadhi ya ajili ya msimu ujao.

na Sebastian Mnakaya

Wananchi wa halmashauri ya ushetu wilayani kahama mkoani Shinyanga wametakiwa kuendelea kuhifadhi chakula ili kuepuka upungufu wa chakula kwa msimu ujao kutokana na mvua zisizokuwa na uhakika.

Wito huo umetolewa na afisa kilimo wa Halmashauri ya Ushetu MAPENZI MSHANA ambapo amesema kuwa wafanyabiashara wengi wamekuwa wakinunua mazao kwa bei ya chini hali inayosababisha wakulima kuuza chakula na kusahau kukihifadhi ya ajili ya msimu ujao

Sauti ya Afisa kilimo

Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri ya Ushetu GAGI LALA amewaomba maafisa kilimo kutoa elimu kwa wakulima namna bora ya kuvuna pamoja na kutunza mazao yao yawe salama kutokana na kuvuna mazao kwa wingi

Sauti ya mwenyekiti wa halmashauri ya Ushetu

Naye, diwani wa kata ya Nyamilangano ROBART MIHAYO amesema kuwa katika kipindi hiki wakulima hawapaswi kuuza chakula na badala yake wakitunze kwa ajili ya familia zao.

Sauti ya diwani wa kata ya nyamilangano