Kahama FM

Wanawake Shinyanga kunufaika na mikopo ya 10%

March 7, 2025, 2:08 pm

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha akitembelea mabanda ya wafanyabiasha wadogo katika maadhimisho ya wanawake dunia yaliyofanyika katika Halmashauri ya msalala mkoani Shinyanga. Picha Sebastian Mnakaya

wanawake watakiwa kuchangamkia fursa za mikopo isiyo na riba inayotolewa na Halmashauri ikiwa na Lengo la kuwainua kiuchumi kuliko kukimbilia mikopo ya kausha damu inayotolewa kwa masharti magumu pamoja na riba kubwa inayopelekea kudidimia kiuchumi

Na Sebastian Mnakaya

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha amekabidhi hundi ya shilingi Bilioni 1.3 kwa halmashauri ya Ushetu zikiwa ni fedha za asilimia 10 kwa ajili ya mikopo kwa Wanawake, Vijana na watu wenye ulemavu.

Akizungumza katika maadhimisho ya Kilele cha Sherehe za Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika kimkoa katika Kata ya Bugalama Halmashauri ya ya Msalala, Macha amewasihi wanawake kuendelea kuchangamkia fursa mbalimbali za kiuchumi ili kuchochea maendeleo.

Aidha Macha amewataka watendaji wa vitongoji, vijiji, mitaa na kata mkoani humo kuwasidia vikundi vya wanawake waliokopa mikopo halmashauri kutoka mapato ya ndani ya asilimia 10% kwa kununua bidhaa mbalimbali wanazozalisha ili kuendelea kuboresha biashara zao.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha

Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Halamshauri wa halmashauri ya Ushetu, Hadija Kabojela ameipongeza serikali chini ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuruhusu fedha hizo kutolewa kwa sababu yalikuwa ni matamanio ya wananchi ya muda mrefu.

INSERT……..DED USHETU

Sauti ya Mkurugenzi wa mtendaji wa Halamshauri ya Ushetu Hadija Kabojela

March 8 kila mwaka dunia huadhimisha siku ya wanawake ambapo kwa mkoa wa Shinyanga maadhimisho hayo yameanza Machi 4 yakiwa na kauli mbiu “Wanawake na Wasichana 2025 tuimarishe usawa nauwezeshaji”