Kahama FM

Madiwani Ushetu waitaka TANESCO Kahama kufikia vijiji vyote

February 9, 2025, 5:05 pm

Mwenyetiki wa halmashauri ya ushetu Gagi Lala akiendelea na kikao cha baraza la madiwani

Baadhi ya maeneo katika halmashauri ya Ushetu hayajapatiwa umeme kutoka na lengo la TANESCO ni kupeleka katika vijiji hivyo maeneo yaliyorukwa mengi ni vitongoji, hivyo baada ya vijiji kufikiwa zoezi la kupeleka kwenye vitongoji litafanyika

Na leokadi Andrew

Madiwani wa Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama mkoani Shinyanga wameliomba shirika la umeme TANESCO wilayani Kahama kupelekea umeme katika vijiji vilivyorukwa na kuweka vifaa maalumu katika taasisi mbalimbali ili kuondokana na ajali za radi zinazoleta athari za vifo pamoja na kubomoa miundombinu.

Hayo yamesemwa na baadhi ya madiwani wa Halmashauri hiyo wakati wa kikao cha baraza la madiwani, ambapo diwani wa kata ya Ulowa Alphonsina Kimaro amesema kuna baadhi ya vijiji havijapatiwa umeme ingawa umeme umepita katika maeneo hayo, huku diwani wa kata ya Ubagwe Robert Lushesha ameomba TANESCO kuweka vifaa vitakavyozuia athari zanazotokana na radi.

INSERT…….MADIWANI USHETU

sauti ya madiwani

Akitoa ufafanuzi juu ya changamoto hizo Meneja TANESCO Halmashauri ya Ushetu Goerge Madaha amesema kwa sasa wanaendelea na kusambaza umeme katika vijiji ambavyo bado havijafikiwa , huku wakiweka vifaa vya kuzia athari za radi kwa baadhi ya taasisi.

sauti ya Goerge Madaha

Katika hatua nyingine, mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Ushetu Hadija Kabojela amewataka madiwani kuwapa taarifa wananchi waliojiandikisha katika zoezi la ugawaji chandaruwa kuwa kuanzia wiki ijayo watapatiwa vyandaluwa hivyo vinavyotewa bure naserikali.

Sauti ya mkurugenzi halmashauri ya Ushetu Hadija Kabojela